Psalms 126

Kurejezwa Kutoka Utumwani

Wimbo wa kwenda juu.

1 a Bwana alipowarejeza mateka Sayuni,
tulikuwa kama watu walioota ndoto.
2 bVinywa vyetu vilijaa kicheko,
ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.
Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,
Bwana amewatendea mambo makuu.”
3 c Bwana ametutendea mambo makuu,
nasi tumejaa furaha.

4 dEe Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa,
kama vijito katika Negebu.
5 eWapandao kwa machozi
watavuna kwa nyimbo za shangwe.
6Yeye azichukuaye mbegu zake
kwenda kupanda, huku akilia,
atarudi kwa nyimbo za shangwe,
akichukua miganda ya mavuno yake.
Copyright information for SwhNEN